Chuo kikuu cha Makere nchini Uganda kimemsimamsha kazi mmoja ya mhadhiri wa chuo hiko kwa tuhuma za kumnyanyasa na kumdhalilisha kimapenzi mwanafunzi wa kike chuoni hapo.

Taarifa hiyo imetolewa na Msaidizi Mkuu wa Chuo hicho Profesa William Bazeyo, ambapo kupitia utomvu huo wa nidhamu Chuo kimemuadhibisha kwa kumsimamisha kazi kwa muda na kumlipa nusu ya mshahara wake.

Katika barua hiyo ya kumsimamisha Mkuu wa Chuo ameandika.

”Nakusimamisha kazi kwa kosa la utomvu wa nidhamu, na kama sehemu ya kutumikia adhabu chuo kitakulipa nusu pesa ya mshahara wako, Aidha unashauriwa kutokuonekana maeneo yeyote ya chuo wala kufanya mazungumzo na mwanafunzi wa Chuo hiki, Utarejeshwa kazini mara tu uchunguzi utakapokamilika juu ya tuhuma zinazokukabili”.

Mwanafunzi huyo alimlipoti Polisi mhadhiri huyo wa chuo akidai kuwa alimshika sehemu zake za siri kwa nguvu bila ruhusa yake.

Auawa kisa wivu wa mapenzi
Manesi 15,000 wasimamishwa kazi