Mwalimu wa kike wa shule moja ya Sekondani katika eneo la Seme nchini  Kenya anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi ya jinsia moja na wanafunzi wa kike.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Kisumu, John Kamau amesema kuwa mwalimu huyo anashikiliwa kutokana na mashtaka yaliyofunguliwa katika kituo cha polisi na wanafunzi wanne wa kike wanaodai aliwafanyia vitendo hivyo.

Wanafunzi hao walioandika maelezo katika kituo cha polisi, wamedai kuwa mwalimu huyo amekuwa wakiwaita nyumbani kwake katika eneo la Kombewa na kuwafanyia vitendo hivyo.

Kufuatia malalamiko hayo, wanafunzi wa shule za bweni na wale wa shule za kutwa waliandamana wakitaka hatua kali zichukuliwe na mamlaka husika dhidi ya mwalimu huyo.

Jeshi la polisi linaendelea kumhoji mwalimu huyo na mashtaka rasmi dhidi yake yatawasilishwa mahakamani, kwa mujibu wa jeshi hilo.

Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na katiba ya Kenya, kama ilivyo kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chanzo: Citizen Kenya

Gazeti la Mwananchi latakiwa kuomba radhi
Video: Makontena 20 ya 'Paul Makonda' yana mali za sh 1.4 bilioni, Wizara tano zaonja joto la jiwe