Kocha aliyetamba na kikosi cha Mbeya City, na aliyewahi kuwa kocha msaidizi timu ya Yanga Juma Mwambusi, ameonesha kusikitishwa na matokeo mabaya katika timu ya Taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars na kutoa maoni yake ambapo amesema, timu ya taifa sio mahali pa kujifunzia ukocha.

“Kinachosikitisha watanzania ni timu yetu kufanya vibaya sana katika mashindano ya Chalenji yanayoendelea kule Kenya. Kubwa kama mwalimu ni kuelezana ukweli, watanzania wanataka matokeo mazuri kitu ambacho kocha aliyeteuliwa na wachezaji lazima wajitume na kujitolea kwa ajili ya nchi yao.”

Aidha Mwambusi ameilaumu TFF kwa kufanya uchaguzi mbovu wa kocha usiozingatia kanuni na taratibu na ametoa ushauri kwa TFF.

”Naishauri TFF kwamba walimu wapo waliofundisha ligi kuu wamefanya vizuri wanatakiwa wapewe nafasi wafundishe timu ya taifa” ameshauri Mwambusi.

Hata hivyoa Mwambusi amechanganua baadhi ya sababu zilizopelekea kocha huyu kushindwa kuingoza vyema timu ya Tanzania bara na kusema kuwa ugeni wake katika soka unaweza kuwa chanzo cha kuifelisha timu hiyo.

”Mwalimu huyu ni mgeni katika soka la Tanzania labda kama alicheza lakini hajafundisha kwa sababu lazima ufundishe vilabu vya ligi kuu ili uweze kuteuliwa mwalimu wa timu ya taifa, lakini sio kufundisha tu umefanya nini katika klabu au vilabu ulivyofundisha. Una wasifu mzuri unawajua watanzania unajua utamaduni wa wachezaji wetu, kwa sababu mwalimu anaweza kuwa mzuri lakini anafundisha katika mazingira yapi na yeye katoka mazingira gani?” amesema Mwambusi.

“Nakumbuka Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi aliwahi kusema “timu yetu imekuwa kichwa cha mwendawazimu” kwa hiyo kuifuta hii kauli ni lazima tufanye vizuri. Inatakiwa timu iwe na mwelekeo.

JPM: Jumuiya tembeeni vifua mbele
Ripoti ya SIPRI yabainisha ongezeko la uuzaji silaha duniani