Beki tegemeo wa Young Africans Bakari Nondo Mwamnyeto amerejea kikosini kuendelea na majukumu yake kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa mkoani Mbeya Jumamosi (Februari 13).

Mwamnyeto ambaye pia ni nahodha msaidizi wa Young Africans, alikuwa na kikosi cha timu ya Taifa nchini Cameroon ambacho kilishiriki michuano Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’.

Ikumbukwe siku chache kabla ya safari ya Cameroon, Mwamnyeto alipata msiba mkubwa wa kufiwa na mchumba wake kutokana na matatizo ya uzazi.

Baada ya kurejea nchini kutoka Cameroon, Mwamnyeto alipewa muda zaidi wa mapumziko, na sasa amerejea kazini kuipigania Young Africans katika kampeni yake ya kusaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu 2020/21.

Mbali na kurejea kikosini Mwamnyeto ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri kuelekea Mbeya, tayari kwa mchezo wa keshokutwa jumamosi dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.

Wakati huo huo mshambuliaji wa Young Africans Saido Ntibanzokiza amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa hawapaswi kukasirika  wala kuchukizwa na maneno ya mitandaoni badala yake watambue kuwa wao kama wachezaji wanajua majukumu yao na nini cha kufanya wanapokuwa uwanjani.

Matokeo ya mechi za Kirafiki yasiwavunje moyo. Tutafanya vizuri kwenye michezo yetu ya ligi. Kikubwa mashabiki wazidi kutusapoti ili tuweze kufanya vizuri kufikia kwenye malengo ambayo tunayahitaji.

Young Africans imjeondoka jijini Dar es salaam leo Alhamisi kuelekea Mbeya, tayari kw amchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.

Zahera: Ninaipa Simba 60%, AS Vita Club 40%
Kaizer Chiefs wasubiri huruma ya CAF, RMFF