Kanisa la Calvary Assembles of God limetoa taarifa kuwa mtume wake na nabii, Boniface Mamposa amepumzika kwa muda hadi pale jeshi la polisi litakapojiridhisha kabla ya kuendele na huduma.

Askofu mkuu wa Kanisa hilo, Dustan Maboya amesema hayo wakati wa ibada maalumu ya maombolezo ya watu 20 waliofariki wakati wa utekelezaji wa imani ya kukanyaga mafuta ya upako katika uwanja wa mpira wa Majengo mjini Moshi.

Amesema kanisa hilo litaendelea na kutoa huduma zake za kitume ikiwemo kukanyaga mafuta ya upako huku wakizingatia tahadhari za kiusalama katika mikutano yote ambayo itaendelea nchini.

Hayo yamejiri ikiwa ni takribani siku nne zimepita tangu jeshi la polisi nchini kuwaachia kwa dhamana watu nane akiwemo nabii Mwamposa ambaye ndiye aliye ongoza kongamano hilo lililosababisha vifo vya watu 20.

Kwa mujibu wa Jeshi la polisi, baada ya kuachiwa kwa dhamana Mwamposa na wenzie wataendelea kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea.

Aidha Mchungaji huyo amesema wamejifunza kitu kikubwa kupitia tukio hilo na kamwe halitojirudia kwani wamepanga kuchukua tahadhari zote za kiusalama.

Amemshukuru Rais John Magufuli kwa busara zake ambazo anaamini zimesaidia kuleta utulivu ” Busara pekee ya Rais wetu, Dkt. Magufuli pamoja na wasaidizi wake imetuvusha salama katika maafa yale, Mungu azidi kumpa hekima yeye na wasaidizi wake”

Kobe na Gianna kuagwa rasmi
WHO yatangaza Dunia inakabiliwa na uhaba vifaa vya kujikinga na Corona