Meneja wa klabu ya Man Utd Jose Mourinho, ametakiwa na chama cha soka nchini Uingereza (FA) kutoa maelezo ya kujitetea kuhusu kauli aliyoitoa siku moja kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Liverpool kuhusu mwamuzi  Anthony Taylor.

Mourinho alizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu uteuzi wa mwamuzi huyo kwa kusema unapaswa kubadilishwa kutokana na shinikizo kubwa lililokua likiendelea baina ya mashabiki wa Man Utd dhidi ya wale wa Liverpool, ambao walikua wakivutana kuhusu Taylor alionekana huenda angeshindwa kutenda haki.

Meneja huyo kutoka nchini Ureno alisema kufuatia hali ilivyokua ikiendelea mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana, ungekua mgumu kwa mwamuzi huyo ambaye alihisiwa huenda angeibeba Man Utd kutokana na asili yake kuwa ya mji wa Manchester.

FA wamembana Mourinho na kumtaka atoe maelezo ya kutetea hoja yake, kwa kutumia kifungu cha kanuni ambazo zinawanyina nafasi mameneja wa klabu kuzungumza lolote kuhusu uteuzi wa waamuzi waliopangwa kuchezesha michezo inayowahusu.

Mourinho mwenye umri wa miaka 53, amepewa muda hadi ijumaa jioni kuwasilisha maelezo ya utetezi wake kwa njia ya maandishi.

Ikulu yakanusha taarifa ya kutenguliwa kwa uteuzi wa RC Gambo
Ziara ya Makamba yatua Maabara ya Chura wa Kihansi, azuru misitu na vijiji Iringa