Mwana FA amekiri kuwa nguvu ya wimbo wa Darassa ‘Muziki’ iliyotoka mwezi uliopita imezipa shida kubwa nyimbo za wasanii wakubwa zilizotoka wakati huu.

FA ambaye ni mmoja kati waliotoa wimbo mpya ‘Dume Suruali’, ingawa wimbo wake umepata mafanikio katika mtandao wa YouTube zaidi ya nyimbo zake zote, amesema kuwa amefarijika kumuona Darassa akifanya mapinduzi kwakuwa kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu wimbo wa rap umezizidi nguvu nyimbo za wasanii wa kuimba wakubwa zilizotoka pamoja.

darassa-muziki

“Kwanza I’m happy for rap music. Imekuwa muda mrefu hatujawahi kutengeneza nyimbo halafu zikatoka na nyimbo za waimbaji, halafu usisikie nyimbo za waimbaji na rap music ndio ikawa vile,” Mwana FA alifunguka jana kwenye FNL ya East Africa TV.

Aliongeza kuwa amefurahi kuona Darassa anafanya vizuri hivi sasa kwani amekuwa akimfahamu miaka mingi iliyopita akihangaika na muziki wake. Amesema alichokifikia Darassa ndio maana halisi ya ‘Usikate Tamaa’.

Wimbo wa Darassa, ‘Muziki’ aliomshirikisha Ben Paul umekuwa wimbo mkubwa kuliko nyimbo zake zote huku ikivunja rekodi ya kukubalika mitaani na mtandaoni kuliko wimbo wowote uliotoka wakati ndani ya kipindi cha miezi miwili ndani ya Tanzania.

Maalim Seif afunguka kuhusu Lipumba ‘kumshawishi’ Lowassa, amsifu Rais Magufuli
Masharti Ligi Kuu Duru La Pili