Hamisi ’Mwana FA’ Mwinjuma amekosoa vikali uamuzi wa kuruhusu nyimbo za Nigeria kutawala shindano la kumsaka mrimbwende wa Tanzania (Miss Tanzania 2016) lililofanyika wikendi iliyopita jijini Mwanza.

Mpishi huyo wa hit ya ’Asanteni kwa Kuja’ ameiambia Ladha 3600 ya E-FM kuwa kitendo cha kuruhusu muziki wa Nigeria kutawala shindano hilo kubwa nchini ni kuuangusha muziki wa Tanzania.

“Unapigaje muziki wa Nigeria kwenye mashindano ya Miss Tanzania..! Ni kwamba haya mamilioni ya nyimbo za kitanzania yote hakuna wimbo mmoja uliofaa kutumika kama Sound track ya mashindano ya Miss Tanzania.. kweli!!?” alihoji Mwana FA.

miss-tanzania

Alisema kuwa kusapoti muziki wa Tanzania kufika katika ngazi za kimataifa zaidi kutawezekana zaidi endapo muziki huo utachezwa kwa wingi ndani ya nchi zaidi ya nyimbo za kigeni.

“Kuna umuhimu wa watu wetu kufanya juhudi za makusudi kabisa kuhakikisha kwamba muziki wetu unapata nafasi zaidi kwetu kuliko muziki wao hapa,” alisema.

Mwana Falsafa alisema kuwa Nigeria walifanya juhudi za makusudi kuhakikisha muziki wao unakuwa na hadi sasa ndio muziki mkubwa zaidi Afrika.

Video: Ziara ya Rais Magufuli Kenya
Video: DC mjema autaja mkakati wake kuhusu machinga Ilala