Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma (Mwana FA), akishirikiana na Marafiki wa Muheza wamezindua Mafunzo maalum ya utawala bora, sheria za umilikaji wa ardhi pamoja na udhibiti wa ukatili wa kijinsia kwa madiwani wa Kata zote za Muheza.

Semina hiyo, iliyodhaminiwa na Taasisi ya Legal Services Facility (LSF) na kuhudhuriwa na Madiwani wote wa Wilaya ya Muheza ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo Madiwani hao kufanya kazi zao za kitawala kwa weledi.

Aidha, Semina hiyo pia inalenga kuwawezesha Madiwani hao kuwapa taaluma ya sheria za ardhi na haki za wanawake katika umilikaji wa ardhi, itakayowasidia katika utatuzi wa migogoro ya ardhi Wilayani humo.

Baleke anaitaka Ligi ya Mabingwa Afrika
Kocha Coastal Union aomba muda