Mbunge wa Jimbo la Muheza Khamis Mwinjuma *MWANA FA*, ameungana na wadau wa Soka mkoani Tanga kuipambania timu yao ya Coastal Union inayowania kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mwana FA ametoa hamasa ya kuhakikisha Coastal Union haishuki, alipoongea kwa njia ya simu na Mlezi wa klabu hiyo Ummy Mwalimu alipowatembelea wachezaji kambini kwao leo asubuhi.

Mwana FA alisema: “Afe kipa afe beki Coastal Union hatushuki daraja.”

Tayari Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Tanga, Wakiwemo Mkuu wa Mkoa, wakuuu wa Wilaya, wabunge  wameungana kuhakikisha wanaibakisha Coastal Union Ligi Kuu Tanzania Bara.

Leo saa kumi jioni Coastal Union itacheza mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya mtoano (Play Off) Ligi Kuu dhidi ya Pamba FC ya jijini Mwanza.

Mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jumatano (Julai 21), Uwanja wa Nyamagana Mwanza, timu hizo zilifungana 2-2.

Coastal Union inapambania kubaki Ligi Kuu msimu ujao, huku Pamba FC ikiwania nafasi ya kupanda daraja ikitokea Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Bashungwa atoa maagizo kwa maafisa michezo
Waziri Ummy aitembelea Coastal Union kambini