Rapa mkongwe, Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amesema kuwa mawazo yaliyojengeka kwa wasanii wengi wa Tanzania kujikita zaidi katika kufanya video kali na nyimbo za kawaida ni kuukosea muziki adabu.

Mwana FA ameeleza kuwa chanzo cha muziki mzuri ni audio yenye mashairi mazuri ambayo hayategemei video pekee kuukuza muziki husika.

FA ambaye jana aliachia kwa kushtukiza wimbo wake mpya uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki unaoitwa Ásanteni Kwa Kuja’, alitoa mtazamo wake akiungana na kile alichokisema Jay Mo kwenye wimbo wake mpya ‘Game’ kuwa wasanii wa sasa wanategemea zaidi video kali kuuza nyimbo mbovu.

“Kuanza kutegemea kwamba hufanyi chochote kwenye muziki halafu unataka video yako ndio ikubebe ni makosa,” FA aliiambia XXL ya Clouds Fm.

“Kwa hiyo mimi niko na Jay Mo… nimefanya video kali sana, lakini nimefanya wimbo mkali zaidi. Na ndio maana naweza kutoa wimbo halafu nikasema video ntaitoa baadae, sina wasiwasi,” aliongeza.

FA aliielezea video yake mpya kuwa ni kali sana kama ulivyo wimbo wake lakini inahitaji kufanyiwa uhariri ili iwe na ‘version’mbili, moja safi itakayoenda kwenye video, na nyingine ‘chafu’ itakayoingia YouTube na kupigwa kwenye kumbi za starehe.

Walioukataa uwaziri wa Magufuli Wafunguka sababu
Kubenea Atiwa Mbaroni kwa Amri Ya Makonda, adaiwa kumkosea adabu