Uongozi wa Klabu ya Simba SC kupitia Kamati ya Uchaguzi imewakumbusha Wanachama wenye nia ya kuwania nafasi za Mwenyekiti na Wajumbe wa ya Wakurugenzi wa Klabu hiyo, kuchangamkia Fursa ya uchuakuaji wa Fomu za kuwania nafasi zilizotangazwa.

Zoezi la Uchuakuaji Fomu za kuwania nafasi za Uongozi ndani ya Simba SC limeanza rasmi leo Jumatatu (Desemba 05) na litafikia ukomo Jumatatu (Desemba 19).

Simba SC imetoa taarifa maalum katika kurasa zake za Mitandao ya kijamii ikiwahimiza Wanachama kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo sambamba na gharama ambazo wanatakiwa kulipia.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa: Fomu zitatolewa kuanzia saa 3 asubihi hadi saa 10 jioni katika ofisi za Klabu zilizopo Polt No 8 na 9 Haile Selasie, Oysterbay jijini Dar es salaam.

Gharama ya Fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti ni Shilingi laki (300,000) na fomu za kugombea nafasi ya Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ni Shilingi Laki moja na Hamsini elfu (150,000).

Jumamosi ya Novemba 26, Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC chini ya Mwenyekiti wake Boniface Lyamwike, ilijokeza hadharani na kutangaza Kalenda maalum ya Uchaguzi ambayo itafikia kilele chache Januari 29 Mwaka 2023.

Akiwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari Boniface Lyamwike alisema: “Mwaka huu kanuni ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa Simba ni kanuni za Simba Sports Club. Huko nyumba tulikuwa tunatumia kanuni za TFF, katiba ya Simba ilikuwa inaruhusu.”

“Kanuni ya sita (kanuni za uchaguzi Simba), kigezo cha kwanza mgombea lazima awe mwadilifu na awe na kiwango cha juu cha uaminifu. La pili lazima awe mwanachama hai wa klabu.”

“Mtu yeyote ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ni lazima awe na angalau shahada ya chuo kikuu, na lazima awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha klabu ndani na nje ya nchi.”

“Anayegombea nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi lazima awe amefika kidato cha nne na cheti za kuhitimu, kigezo kingine awe mzoefu uliothibitishwa wa angalau miaka mitatu ya uongozi wa mpira wa miguu.”

“Kingine asiwe amepatikana kamwe ya hatia ya kosa ya jinai, lakini pia angalau awe na miaka 25 na si zaidi ya miaka 64, lakini pia asiwe mmiliki, mwanahisa au kiongozi wa timu ngyine ya mpira wa miguu.”

“Nafasi ambazo zitagombewa ni mwenyekiti nafasi moja, kutakuwa na mjumbe wa pili lakini pia kutakuwa na wajumbe wengine wanne. Jumla zitakuwa nafasi sita.”

“Katiba inampa nafasi mwenyekiti atakayechaguliwa kuchagua wajumbe wengine wawili. Lakini pia kuna kigezo cha msingi sana, katika nafasi nne, angalau mmoja au zaidi awe mwanamke.”

Charles Mkwasa ajing'oa Ruvu Shooting
Arsenal, Liverpool zaalikwa Falme za Kiarabu