Mwanafunzi wa chuo cha IFM mwaka wa tatu, Robson Isack Maji mkazi wa Segerea anashikiliwa na polisi baada ya kukutwa na bastola aina ya Beretta ikiwa na risasi 6 ndani ya magazine.

Robson amekiri kutumia bastola hiyo kibiashara ambapo amekuwa akikodisha kwa majambazi kufanyia uhalifu na kulipwa fedha.

Polisi walipata tetesi juu ya harakati hizo za majambazi kukodi silaha na kufanyia uhalifu, ndipo walipoanza kufuatilia na kumnasa mwanafunzi Robson.

Polisi walimuhoji Robson alipoipata silaha hiyo, naye alidai kuwa aliiba kwa baba yake mzazi anayejulikana kwa jina la Isack Maji.

Tayari polisi wanamshikilia Isack Maji kwa kosa la kumili silaha, pia imebahinika kuwa hana umiliki halali wa silaha hiyo.

Pia Polisi inamshikilia Patrick Makai ambaye alitajwa na mwanafunzi Robson kuwa amekuwa akishirikiana naye katika biashara hiyo ya kukodisha bastola kwa majambazi.

 

Fid Q kuyaanika maisha yake kwenye kitabu, albam
Wivu wamponza mke atiwa mbaroni