Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Sabasaba iliyopo jijini Mwanza, Dotto Baraka (13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri ya simu aliyokuwa akiiunganisha na radio chakavu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa limetokea Mei 17, mtaa wa Igoma Mashariki jijini humo.

“Baada ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza kutengeneza radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha kwenye nyanya za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na kusababisha kifo chake,” amesema Kamanda Msangi.

Hata hivyo, Kamanda Msangi ameongeza kuwa wakati tukio hilo linatokea, wazazi wa watoto hao walikuwa safarini huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Maaskofu 34 Chile wataka kujiuzulu
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Uruguay