Mwanafunzi wa Misri Ahmed Bassem Zaki (22) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kuwanyanyasa kijinsia wanawake wawili kupitia mitandao ya kijamii.

Mahakama inayoshughulikia Uhalifu wa Kimtandao, ilimkuta Mwanafunzi huyo na hatia ya kutuma picha na jumbe zenye maudhui ya ngono kwenye simu za wanawake.

Kwa mujibu wa sheria za Misri, unyanyasaji wa Kijinsia ni kosa kisheria tangu mwaka 2014, na mashtaka dhidi ya Zaki yalichochea kwa kiasi kikubwa Kampeni ya MeToo ambapo wanawake walijitokeza kuripoti matukio hayo.

Kesi hiyo ilipata umaarufu Misri ambapo Wanaharakati wa Haki za Wanawake wanadai unyanyasaji wa kijinsia ni janga kubwa ambalo halipewi uzito.

KMC FC kuifuata Mbeya City
Ndejembi: Fufueni mashamba ya zabibu