Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi, ameagiza kupimwa mimba kwa wanafunzi kwa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kiangara iliyopo mkoani humo, baada ya mmoja wa wanafunzi hao kudaiwa kujifungua nyuma ya darasa.

Zambi ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara shuleni hapo, ili kujua maendeleo ya wanafunzi wanaofanya mtihani wa kidato cha pili.

Ambapo mkuu wa mkoa alikutana na taarifa hizo za mwanafunzi kujifungua nje ya jengo la Shule wakati mitihani ikiendelea.

“Nimepata habari za kushtua kidogo, kwamba kuna mwanafunzi wakike amejifungua jana hapa shuleni hii ni aibu kubwa sana kwenu kwa watoto wakike, huu Mkoa wetu tulishakuwa na oparesheni ya kutokomeza mimba.” amesema Zambi

“Nitawachukua wanafunzi wote nyinyi mkishafungua Shule tu wote muende mkapime kama hamna mimba au hamjawahi kutembea na wanaume na waagiza walimu msimamie hili” ameongeza Zambi.

Tangu mwezi Januari hadi Julai 2019, zaidi ya wanafunzi 75 wa Shule za Msingi na Sekondari mkoani Lindi, wamebainika kuwa na mimba.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 20, 2019
Video: Meya Kinondoni azindua mashindano ya kuvua

Comments

comments