Jeshi la polisi nchini Zambia linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu kwa tuhuma za kumkashifu Rais Edgar Lungu na maafisa wengine wa Serikali kwenye Facebook.

Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo, Esther Katongo amesema kuwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 35 aliyetajwa kwa jina la Edward Makayi amedaiwa kufungua ukurasa wa Facebook kwa jina ‘feki’ na kuutumia kumkashfu Rais Lungu.

Katongo alieleza kuwa mtuhumiwa huyo pia aliutumia ukurasa huo kwa muda mrefu kuwakashfu na kuwatukana mawaziri wa Serikali ya nchi hiyo, viongozi wa chama tawala, msemaji wa Rais Lungu na mkuu wa jeshi la polisi la Zambia.

Msemaji huyo wa jeshi la polisi amesema kuwa mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na kwamba atafikishwa mahakamani Alhamisi (leo).

Hata hivyo, mwanasheria wa mtuhumiwa huyo hakuzungumza lolote kuhusu mashtaka yanayomkabili mteja wake.

Video: Lowassa alonga miaka miwili ndani ya upinzani, Makanikia yaivuruga Acacia
Wajawazito wafa maji wakijaribu kutoroka