Mwanafunzi  wa darasa la tano shule ya msingi Kibeta mkoani Bukoba, Sperius Eradius (13),  aliyeuawa kwa kichapo Agosti 27 mwaka huu tayari amezikwa katika kijiji cha kitoko kata ya Mubunda wilayani Muleba.

Serikali imehudhuria mazishi hayo na kuwakilishwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kandege ambaye alitoa salamu za serikali.

Akizungumza katika mazishi hayo Kandege amesema Serikali itasimamia haki ya mwanafunzi huyo mpaka ipatikane na kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

Hivyo Kandege alikabidhi shilingi Milioni 2 kwa niaba ya serikali na kusema kwamba pamoja na hayo yote hawawezi kukubali jambo hilo lipite lazima iwe fundisho kwa walimu wengine wanaoachiwa dhamana na wazazi wawafundishe watoto wao.

Aidha baba mzazi wa marehemu alisema yote yaliyotokea anamwachia Mungu pia ameishukuru serikali kwa kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu tangu mwanzo hadi sasa wanapompumzisha kwani serikali imekuwa ikigharamia mahitaji yote katika familia ya baba mlezi, tangu kutokea kwa msiba huyo lakini pia imegharamia jeneza na usafiri kuelekea Muleba kwenye mazishi.

Marehemu Sperius Eradius (13),  kifo chake kimesababishwa na adhabu kali aliyopewa na mwalimu wake wa nidhamu baada ya kumpokea mzigo mwalimu Herieth Gerald na baadae kutuhukiwa kuiba pochi ya mwalimu huyo, kwa mujibu wa baba mlezi marehemu alikuwa mchangamfu, mcha Mungu na mwimbaji kwaya.

Walimpenda ila Mungu amempenda zaidi apumzike kwa amani.

 

 

Video: Gari la watalii lapata ajali mbaya Arusha
‘Kutoonekana’ makontena 10 ya Makonda mnadani kwazua jambo