Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mbeya, Sebastian Chinguku ambaye alionekana kwenye kipande cha video kilichosambazwa mitandaoni akipigwa kikatili na walimu wa mafunzo kwa vitendo, amesema kuwa kipigo hicho cha kikatili hakikuishia hapo.

Walimu walioshiriki kumpiga mwanafunzi huyo ni Frank Msigwa (Chuo Kikuu cha Dar es Salam), John Deo (Chuo Kikuu cha Dar es Salam), Evance Sanga (Chuo Kikuu cha Dar es Salam) na Sante Gwamaka (Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere).

Mwanafunzi Sebastian Chinguku

Mwanafunzi Sebastian Chinguku

Mwanafunzi huyo amesema kuwa sauti ya mwalimu wa kike iliyokuwa ikisikika kwenye video hiyo ilipelekea walimu wale kumuacha kwa muda, lakini walimtoa katika ofisi ya walimu na kumrudisha darasani ambapo walimpiga tena kikatili.

“Waliniadhibu tena mbele ya wanafunzi kwa mara nyingine tena,” anasimulia. “Kwanza wakati tunatoka ofisini, nilimwambia mwalimu kwakuwa mmenichapa sana na mwili wangu wote unauma naomba basi mnipe adhabu nyingine hata ya kuchimba shimo… lakini walikataa wakanibeba wakawa wananirudisha tena darasani,” alisema.

Chinguku anasema baada ya kuona walimu wanaendelea kumpeleka darasani kwa lengo la kumpiga tena aliamua kutimua mbio kujinusuru kabla hajafikishwa darasani lakini alikamatwa tena na kufikishwa darasani.

“Nilipofika darasani wakaniambia nikae chini, nilipokaa dakika chache tu mwalimu yule [mwalimu Frank] akanirudia tena mbele ya wanafunzi akanipiga teke sehemu ya jicho, jicho likawa limevimba na kukawa na mchubuko ukawa unatoka damu na nikawa natoka damu puani na mdomoni,” Mwanafunzi huyo aliiambia Ayo TV.

Walimu hao wanne waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo shuleni hapo wameshafukuzwa katika vyuo vikuu walivyokuwa wanasoma na jeshi la polisi linaendelea na utaratibu wa kisheria dhidi yao.

DC Ndejembi akifungia chuo cha ualimu Nkuruma-mkoka
Video: Chris Brown awasili Kenya, Wananchi wataka afukuzwe kama Koffi Olomide.....