Utafanya nini endapo utafika kwenye ATM kuangalia salio ukiwa umebanwa na matatizo lukuki huku salio linasuasua halafu ghafla unagundua akaunti yako ina shilingi bilioni 10? Mwenzako kafanya hivi…

Mwanafunzi mmoja wa kike nchini Australia mwenye umri wa miaka 21 anashikiliwa na vyombo vya usalama nchini humo kwa tuhuma za kutumia mabilioni ya fedha ndani ya mwaka mmoja baada ya kugundua amewekewa kimakosa zaidi ya shilingi bilioni 10 kwenye akaunti yake ya benki ya Westpac.

Lee C

Msichana huyo aliyetajwa kwa jina la Christine Lee, anatuhumiwa kwa kutokuwa mwaminifu baada ya kugundua amewekewa kimakosa  dola milioni 4.6 (sawa na shilingi 10,072,160,000 za Tanzania).

Imeelezwa kuwa alitumia mabilioni kununua vitu vya anasa na kufanya matanuzi ndani ya muda mfupi na kwamba ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tayari alikuwa ametumia $milioni 3.3 (zaidi ya bilioni 7 za Tanzania).

Lee

Christine Lee,

Lee alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Sydney akijaribu kuelekea nchini kwao Malaysia.

Kwa mujibu wa Nines News, Lee alikuwa akiishi kifahari katika jiji la Sydney akilipia pango la nyumba $3120 kwa mwezi (zaidi ya shilingi milioni 6 za Tanzania). Pesa nyingi alitumia katika kununua nguo pamoja na mikoba ya kike.

Msichana huyo alipandishwa kizimbani Alhamisi kujibu mashtaka yanayomkabili.

Machinga kutimulia kona zote Dar
Magufuli kuwagawia wananchi sukari bure