Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza wa shule ya sekondari Mbabala iliyopo mjini Dodoma aliyetajwa kwa jina la Helena Mpondo, amejifungua mtoto ndani ya bweni la shule hiyo.

Ripoti kutoka Dodoma zimeeleza kuwa mwanafunzi huyo alifanikiwa kujifungua salama baada ya kusaidiwa na walimu wa kike waliokuwa shuleni hapo na baadae mganga wa zahanati ya karibu alifika na kumkata mtoto kitovu.

Akizungumzia tukio hilo lililotajwa kutokea Septemba 2 mwaka huu, Mkuu wa Shule hiyo, Joram Mkwawa alisema kuwa baada ya kutaarifiwa kuwa kuna mwanafunzi alikuwa anajifungua bwenini, alifika katika eneo la bweni hilo na kukuta tayari amejifungua.

Alisema kwakuwa alifahamu ni kosa mwanafunzi kukaa na ujauzito shuleni, aliwaita wazazi wake na kuwakabithi mtoto wao baada ya kupata huduma stahiki.

“Wazazi wake walipofika niliwakabidhi mwanae kwakuwa nafahamu ni kosa kwa mwanafunzi kukaa shuleni akiwa na ujauzito,” alisema mwalimu Mkwawa.

Hivi karibuni, Serikali ya Wilaya ya Dodoma ilisema kuwa wilaya hiyo ina wanafunzi 51 wa shule za msingi na sekondari wana ujauzito.

Bodi ya mikopo yawatendea haki wanafunzi wa elimu ya juu kwa mara ya pili.
Picha: Diamond awapeleka WCB kwa JK