Mwanafunzi wa Tanzania aliyekuwa akisoma nchini Afrika Kusini, Baraka Nafari aliyekuwa akichukua Shahada ya Uzamivu (PHD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) ameuawa kikatili Ijumaa Februari 23, mwaka huu kwa kugongwa na gari mara mbili na kubamizwa kwenye ukuta na baadaye kushambuliwa kwa visu.

Kwa mujibu wa habari hizo za mtandao, kamera za usalama za CCTV za chuo hicho zilionyesha Baraka na mwanafunzi mwenzake wakikimbia kujiokoa wakati watu wawili waliokuwa kwenye teksi walipokuwa wakiwakimbiza.

Aidha, Kamera hiyo iliendelea kumuonyesha dereva teksi huyo akimgonga kwa makusudi mwanafunzi huyo kwenye uzio wa makazi ya chuo hicho yaliyoko Auckland Park na kumuua.

Taarifa hizo zimeongeza kuwa dereva wa gari hilo alikamatwa na polisi kwa kuendesha bila leseni, lakini baadaye aliachiwa huru bila kufunguliwa mashtaka yoyote.

Hata hivyo, Msemaji wa Wizara ya Mambo na Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga amesema kuwa wizara inafanya mawasilianao na ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ili kubaini undani wa suala hilo.

 

Reli ya Juu kuanzia Shaurimoyo jijini Dar
Wema Sepetu: Nikisema Makonda ni mtumishi wa Mungu namaanisha