Mtangazaji wa redio ya jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo (DRC), Papy Mumbere Mahamba, ameuawa nyumbani kwake katika eneo la Lwemba, Kaskazini Mashariki mwa Mkoa wa Ituri na Mke wake kujeruhuwa huku nyumba yao ikichomwa moto.

Msemaji wa Jeshi la congo, Jenerali Robert Yav amesema washambuliaji wasiojulikana waliingia nyumbani kwa mtangazaji huyo na kumuua.

Tayari watu wawili wanaohusishwa na mauaji hayo yaliyotekea siku ya Jumamosi, wanashikiliwa na polisi huku chanzo kamili cha mauaji hayo kikiwa bado hakija julikana na uchunguzi unaendelea.

Imeelezwa kuwa kabla ya kuuawa mwandishi huyo aliyejikita zaidi katika kupambana na vita dhidi

Serikali ya nchi hiyo kupitia wizara ya Afya ikishirikiana na mashirika ya kimataifa yanayohusika na mapambano dhidi ya ugonjwa huo wa Ebola wamelaani vikali mauaji hayo.

Ikumbukwe kuwa , watu wengi nchini humo wamekuwa wakiamini kuwa Ebola ni njama ya uongo, kuwa ni kitu kinachobuniwa na wataalamu wa matibabu ili wapate kazi za mishahara mikubwa hivyo  watu wanaofanya kazi ya kukabiliana na ugonjwa huo mara kwa mara wamekuwa wakiuawa na kujeruhiwa.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 5, 2019
Vyama vya ushirika Singida vyahimizwa kukabiliana na wadudu