Mwanahabari wa Shirika la Habari la Marekani Fox News Pierre Zakrzewski ameuawa baada ya kushambuliwa akiwa kazini nchini Ukraine.

Taarifa za Fox News zinasema Mwanahabari Zakrzewski raia wa Ireland mwenye umri wa miaka 55 alikuwa kazini na mwanahabari mwenzake wa Fox News Benjamin Hall gari lao lilipopigwa katika shambulizi la Urusi katika jiji kuu ya Ukraine, Kyiv.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Fox News Suzanne Scott alisema katika ujumbe kwa wafanyakazi wa shirika hilo na kuongeza kuwa Hall amelazwa hospitalini akiwa na majeraha.

Zakrzewski ni mwanahabari wa pili kuuawa akifuatilia mzozo kati ya Ukraine na Urusi, baada ya Brent Renaud, raia wa Marekani, kupigwa risasi na vikosi vya Urusi siku ya Jumapili.

Zakrzewski, raia wa Ireland, alikuwa mpiga picha hodari katika maeneo ya vita ambaye alijijengea sifa kwa kunasa picha nzuri kwa faida ya Fox News katika mataifa ya Iraq, Afghanistan na Syria.

Haya yanajiri huku Wamarekani mashuhuri wakipigwa marufuku ya kuingia nchini Urusi wakiongozwa na Rais Joe Biden, aliyekuwa Katibu wa Serikali ya Marekani Hillary Clitton, Katibu wa sasa ntony Blinken, Katibu wa Ulinzi Lloyd Austin, Katibu wa Mawasiliano ya Ikulu ya White House Jen Psaki na mwanawe Biden, Hunter.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CBS News, Urusi vilevile itafungia mali za wale wote waliotajwa katika orodha hiyo. Urusi nayo imeshikilia kuwa inapanga kuweka vikwazo zaidi katika siku za usoni, vikwazo hivi vikilenga wafanyabiashara na watu katika vyombo ya habari.

Serikali yazindua mfumo wa utoaji kibali kwa wasanii kidigitali
Biden azuiliwa Urusi