Aliyekua nahodha na mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Simba ‘Simba Queens’ Mwanahamisi Omary, amefunguka kuhusu mazingira ya soka la wanawake nchini Morocco, ambapo amekwenda kucheza soka la kulipwa.  

Mwanahamisi aliondoka nchini mwanzoni mwa mwezi huu, baada ya dili lake la kusajiliwa na klabu ya Chabab Atlas kukamilika kwa asilimia 100, akitokea ‘Simba Queens’ ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya wanawake Tanzania Bara.

Mwanahamis amesema:  “Kitu cha harakaharaka ninachoona kipo tofauti na Tanzania, uwekezaji ni mkubwa sana kwenye soka la wanawake, hicho ndicho kinachowafanya waonekane wapo juu, ingawa nyumbani kuna vipaji vikubwa kama vitapata nafasi vinaweza vikafanya vizuri zaidi huku,”

“Nidhamu yao ya kazi ipo juu sana kwa maana ya kujituma na mazoezi binafsi kila mchezaji akitamani kufanya kazi zaidi ya mwingine bila kulazimishwa ama kuhamasishwa na kocha, wamechukulia ni kazi ya heshima na sina maana kwamba kwetu Tanzania haipo hivyo,” amesema na ameongeza kuwa

“Kiukweli najifunza mengi kwa kuangalia mazingira yao, jinsi wanavyojitazama mbali katika kazi yao, hawajichukulii poa, wanajiwazia makubwa kama soka la wanaume, hii itanifanya nipambane sana ili niwe njia ya wengine kupata nafasi huku,”

Itumeleng Khune kuondoka 'AMAKHOSI'?
Namungo FC yaiwekea mikakati Nkana FC