Mmiliki wa kampuni ya habari ”Next Digital” na mwanaharakati wa nchini Hong Kong, Jimmy Lai amekamatwa chini ya sheria mpya ya usalama iliyoanzishwa kwenye jiji hilo.

Msaidizi wake wa karibu Mark Simon amesema kuwa Lai amekamatwa mapema leo akishukiwa kula njama na vikosi vya kigeni.

Kwa mujibu wa gazeti la Apple Daily linalochapishwa na kampuni ya Next Dital imeripoti kuwa Lai, alichukuliwa kutoka nyumbani kwake Ho Man Tin mapema leo pamoja na mtoto wa Lai, Ian naye alikamatwa akiwa nyumabani kwake.

Mwanaharakati huyo mashuhuri ni wa kwanza kukamatwa hadi sasa chini ya sheria hiyo mpya ya usalama ya Hong Kong.

Sheria hiyo mpya inazuia kile ambacho Beijing inakichukulia kama kujitenga na shughuli za kigaidi ama kile inachokiona kama uingiliaji wa nje katika mambo ya ndani ya Hong Kong.

Mahakama yabariki miaka 20 jela kwa kigogo wa dawa za kulevya
DC mpya Ilala afunguka