Mchezaji wa mchezo wa baiskeli nchini Afrika kusini ashambuliwa na msumeno kwenye mguu wake na watu wanao zaniwa kuwa ni wezi mapema jana, jumanne.

Mwanamichezo huyo,  Mhlengi Gwala (26) anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kufuatia tukio hilo lililoleta huzuni miongoni mwa mashabiki wa mchezo huo

Gwala amesema kuwa  alishambuliwa  na wanaume watatu wakati akifanya mazoezi karibu na chuo kikuu cha Zulu-Natal, Darban, Afrika Kusini.

Imeelezwa kuwa wanaume hao walimfatilia na kumvuta kwenye eneo lenye vichaka na kisha kujaribu kumkata mguu lakini alifanikiwa kuwaponyoka waharifu hao.

Gwala anasema alijaribu kuwapa vitu alivyo kuwa navyo ikiwemo baiskeli aliyokuwa akifanyia mazoezi ili wasimdhuru lakini ilishindikana.

Gwala amekuwa ni mwana michezo anaye tabiriwa kufika mbali katika mchezo wa mbio za baiskeli na tayari ameshaanza kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa.

JPM awapongeza wanawake wote
Jerry Muro: Tusiruhusu ushabiki uondoe uzalendo wetu, Hongera Swahiba