Mwanamitindo maarufu nchini Rwanda, Alexia Mupende (35), ameuawa na mfanyakazi wao wandani nyumbani kwa baba yake Nyarugunga wilayani Kicukiro nchi Rwanda.

Taarifa za kifo chake cha ghafla zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii majira ya saa tatu usiku, kwa wananchi kumtafuta muuaji, kijana mwenye umri wa miaka 23 ambaye ni mfanyakazi wa ndani wa nyumba yao.

Taarifa za kutoka vyanzo vya karibu kutoka familia ya Alexia zinaonesha kuwa mipango ya harusi yake ilikuwa imeshaanza na alitakiwa kuolewa mwezi ujao.

Licha ya kuwa mwanamitindo Alexa alikuwa meneja mkuu wa kituo maarufu  cha kufanyia mazoezi cha Waka Fitness mjini Kigali.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo msemaji wa kitengo cha upelelezi, Modeste Mbabazi amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo na sasa hawawezi kutoa taarifa zaidi hadi upelelezi utakapo kamilika na kuhakikishia umma kuwa upelelezi bado unaendelea.

Mwanadada Alexia atakumbukwa sana kwa kutangaza mavazi ya Rwanda  katika majukwaa ya maonyesho ya kimataifa ambapo hivi karibuni alishiriki katika maonesho nchini India na Sri Lanka ambayo yalibeba ujumbe wa ‘Kujali Utu’.

Ikumbukwe kuwa Januari 3, Alexia aliandika ujumbe katika mtandao wa Twitter kuwa mwaka huu ameamua kuwa karibu zaidi na Mungu.

 

 

Video: Mwijaku achambua kilio cha MCPilipili , ‘aliwahi kuniambia...’
Tanesco yatoa tahadhari kwa wakazi wa Dar, Pwani na Zanzibar

Comments

comments