Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la May Chen mwenye umri wa miaka 28 kutoka Taiwan amejioa mwenyewe baada ya kusubiri mchumba kwa muda mrefu.

”Nimekuwa nikisubiri mtu kujitokeza na kusema kwamba angependa kufunga ndoa nami mbali na kupiga picha za harusi nami” amesema May Chen.

Mwanamke huyo (May Chen) ambaye anaugua saratani ya matiti amewagusa watu wengi ulimwenguni kufuatia tendo lake hilo ambalo yeye mwenyewe amesema kuwa ameamua kuafikia ndoto yake kwani hawezi kukubali ugonjwa huo kuwa sababu ya kuhujumu ndoto yake ya kuolewa.

May Chen amesema kwamba wakati unapohisi kwamba huna miaka mingi ya kuishi huna budi kujifanyia maswala ambayo yamekuwa ndoto yako.

Licha ya kuwa wapiga picha walimshauri kupiga picha katika studio lakini yeye akawaambia kwamba anataka picha sawa na zile za harusi, hivyo basi alikodisha gari na kwenda kupiga picha hizo katika maandhari ya harusi.

”Nilipovalia rinda la harusi nilijawa na hisia mpaka nikahisi kulia” amesema

Wakati akizungumza na BBC, May Chen amesema kwamba alihisi kana kwamba ameafikia ndoto yake ya miaka mingi. Kwa sababu anaugua saratani ya matiti hulazimika kwenda hospitali mara tatu kwa wiki ili kudungwa sindano mbali na kutibiwa kwa kutumia kemikali.

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Mei 15, 2017
Prof. Mukandala awaasa vijana, Asema utu, maendeleo na maisha bora havipatikani kwa fedha

Comments

comments