Katika hali ya kustaajabisha mwanamke mmoja nchini Italia amejioa yeye mwenyewe na kufanya sherehe akiwa na vazi kamili la harusi, keki na wageni 70.

Mwanamke huyo anayeitwa Laura Mesi mwenye umri wa miaka 40 amesema anaamini kuwa kila mmoja ni lazima ajipende mwenyewe.

Laura anasema kuwa suala la kujioa alilipata miaka miwili iliyopita, baada ya miaka12 ya kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

 

“Niliwaambia marafiki zangu na familia kuwa sijapata mpenzi na nikiwa na umri wa miaka 40 nitajioa ikiwa siku moja nitapata mwanamume ambaye nitapanga kuishi naye nitafurahi, lakini furaha yangu haimtegemei yeye,” aliliambia gazeti la La Repubblica.

Laura Mesi and her bridesmaids

Laura Mesi anasema kuwa yeye ndiye mwanamke wa Kwanza nchini Italia kufanya harusi ya mtu mmoja wakati watu wengine wakiwa na maoni tofauti juu jambo hilo, wengine wanapinga kitendo hicho huku wengine wakisema amechanganyikiwa.

Hata hivyo Bi Mesi ametupilia mbali maoni hayo akisema hakuna mtu atazima tabasamu lake.

Tunda la kusherehekea ndoa ya Laura Mesi

Uamuzi wa kamati ya bodi ya uendeshaji na usimamizi wa ligi
Kenyatta amtolea uvivu Raila, amtaka ajiengue au ...!