Mahakama ya juu katika jimbo la Kano nchini Nigeria imeanza kusikiliza kesi dhidi ya mwanamke mwenye umri wa miaka 30 ambaye alikamatwa akiweka dawa za kulevya kwenye nyumba ya Mchungaji.

Mwanamke huyo alikamatwa na Maafisa wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini humo, baada ya kudokezwa kuhusu nia ovu ya mwanamke huyo dhidi ya mchungaji ambaye alikuwa jirani yake.

Kamanda Mkuu wa Mamlaka hiyo inayojukana kama National Drug Law Enforcement Agency (NDLEA), Hamza Umar alimtaja mwanamke huyo kwa jina la Joy Ogundare akieleza kuwa alikamatwa katika eneo la tukio akitekeleza nia yake akiwa na gramu 2.2 za Cocaine akiweka nyumbani kwa Mchungaji Richard Ekenne.

Mwanamke huyo amekiri kosa lake na kueleza kuwa alichukua uamuzi huo kwakuwa alikuwa haelewani na Mchungaji Ekenne kwa muda mrefu.

“Nilikuwa sina maelewano na Mchugaji Ekenne. Hadi sasa tuna kesi inayoendelea katika Mahakama nyingine hapa Kano. Ndio maana nilitaka kumuwekea dawa za kulevya nyumbani kwake lakini bahati mbaya nilikamatwa na NDLEA kabla sijakamilisha,” alisema mama huyo.

Kwamujibu wa gazeti la Daily Trust la nchini humo, Mamlaka hiyo imeeleza kuwa itaendelea na kesi hiyo hadi Mahakama itakapotoa uamuzi wake kisheria. Imetahadharisha watu wenye nia na vitendo viovu kama hivyo.

 

Rais Akataa kuishi Ikulu akidai kuna ‘Mizimu na Mashetani’
Video: Mjusi wa Tanzania Aliyepelekwa Ujerumani Atua Bungeni, Mbunge Afichua Haya