Mwanamke wa Indonesia aliyekuwa amepotea amepatikana akiwa amekufa, ndani ya tumbo la chatu mwenye urefu wa futi 23.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya nchi hiyo, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Wa Tiba mwenye umri wa miaka 54, kwa mara ya mwisho aliaga kuwa anaenda kuchuma mboga kwenye bustani yake katika kijiji cha Muna, katikati ya Indonesia.

Mwili wa Wa Tiba ulipatikana Ijumaa iliyopita kwenye tumbo la chatu huyo, umbali wa hatua 50 kutoka kwenye bustani yake ya mboga.

Jakarta Post imeripoti kuwa wanakijiji walikusanyika na kumuua chatu huyo na kufungua tumbo lake, ndipo walipofanikiwa kuutoa mwili wa mwanamke huyo.

“Kwanza walibaini kuwa kuna chatu katika eneo hilo, walipomuua na kukata tumbo lake waliukuta mwili wa Tiba akiwa bado kwenye nguo zake,” mwenyekiti wa kijiji hicho, Faris anakaririwa na Jarkata Post.

Hili ni tukio la pili kutokea nchini Indonesia, ambapo Machi mwaka jana, mwili wa mwanaume mwenye umri wa miaka 25 alikutwa ndani ya tumbo la chatu.

Chatu humshambulia binadamu au mnyama kwa kumzunguka na kumbana mbavu hadi anapopoteza fahamu, kisha kummeza mzima.

Mauzo ya rapa aliyepigwa risasi yapanda asilimia 1600 kwa siku
Makamba azua gumzo na 'kanuni' za kutumia lifti za majengo marefu

Comments

comments