Mwanamke mwenye umri wa miaka 41( Elizabeth Nalem )ambaye ni Afisa wa Mji wa Makutano Pokot Magharibi nchini Kenya,amewashangaza wengi baada ya kutangaza kuwa amefunga ndoa na Roho Mtakatifu.

Harusi hiyo iliyoandaliwa kwenye hoteli ya Chelang’a mjini Makutano ilihudhuriwa na wapambe wa Bibi harusi huyo na kuongozwa na Kasisi Albert Rumaita wa kanisa la Full Gospel.

Akiwa amepambwa kwa mavazi rasmi ya harusi mwanamke huyo mwenye watoto sita alikula kiapo cha kumpenda na kumtumikia huyo mumewe mpya (roho mtakatifu )maisha yake yote.

Aidha Mumewe aliyefahamika kama Joshua Nalem alikuwa ni kati ya mashuhuda wa harusi hiyo amesema haamini kama mkewe aliyeishi naye kwa miaka 20 angefanya tukio kama hilo.

“Nimeshangaa sana. Nilitoa mahari; ng’ombe 22 na mbuzi 15 nilipooa mke wangu. Lakini sasa anafunga ndoa na mume mwingine anayedai kuwa roho mtakatifu,” Amesema Joshua.

Bibi harusi Elizabeth amesema kuwa ameagizwa na Roho Mtakatifu kumtumikia Mungu kwani ameshatumiakia dunia kwa kipindi kirefu sasa toka kuzaliwa kwake.

“Roho Mtakatifu alinituma kwa Pasta Rumaita ambaye alininunulia vazi la harusi, aliandaa hafla hii na akakodisha magari yaliyotuleta hapa,” Amesema Bibi harusi Elizabeth.

Hata hivyo Elizabeth alikiri kuwa kabla ya kuandaa sherehe hiyo iliyotawaliwa na vigeregere na nderemo nyingi aliomba ruhusa kwa mumewe ambaye alikataa jambo hilo.

Serikali yakagua mkongo wa taifa bandari ya Mtwara
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 12, 2021