Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Chloe Haines (26) ambaye alijaribu kufungua mlango wa ndege katikati ya safari Juni 2019, amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Chloe Haines (26) alikuwa akisafiri kuelekea nchini Uturuki, na inaelezwa kuwa alikunywa pombe na madawa kabla ya safari hiyo.

Akiwa kwenye ndege alipiga kelele akisema, “ninataka kufa na nitawaua wote,”; kabla ya kujaribu kufungua mlango wa dharura wa ndege ambapo alidhibitiwa na wahudumu na ndege hiyo ililazimika kukatisha safari na kumrudisha Uingereza.

Hata hivyo, mbali na kupewa hukumu hiyo ya kifungo cha jela miaka 2, Chloe pia amezuiliwa kupata huduma ya kusafiri na ndege hiyo maisha yake yote.

Kampuni ya Ndege aliyokuwa akisafiria, Jet2 mbali na kumfungia maisha huduma, pia imedai kulipwa faini ya Dola 110,000 (Sawa na Tsh. 254,100,000) kwa usumbufu uliojitokeza.

Mwanasheria wake, Oliver Saxby QC amesema mbali na kulewa, Haines hakuwa sawa kiakili wakati anafanya tukio hilo na anajutia kile kilichotokea

Bwawa la nyumba ya Mungu hatarini kupasuka
Wanafunzi watano waliofariki kwa kugongwa na gari wazikwa leo