Mwanamke mmoja raia wa Mali, Halima Cisse, (26) ambaye mwezi Mei alijifungua watoto tisa kwa mkupuo mmoja amewaonyesha sura za watoto wake hao ambao watano ni wa kike na wanne wa kiume.

Halima alijifungua katika kliniki ya Ain Borja, Mjini Casablanca, Morocco, ambapo watoto wake hao waliwekwa kwenye mashine maalumu ya uangalizi hadi mwezi Agosti walipotolewa.

Hata hivyo Halima na mume wake Kader Arby, (35) wamesema japo ni furaha kuwana watoto lakini bado wanawaza namna ambavyo wataweza kujipanga kimaisha ili kuweza kuwalea pacha hao tisa na mwenzao mmoja ambao ni jumla ya watoto 10, licha ya serikali ya Mali kuwasaidia kulipa gharama za hospitalini.

Halima Cisse amevunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Nadya Suleman ambaye alizaa watoto wanane mwaka 2009.

Meek Mill ahofia kutapeliwa
Ushahidi wa Wazi Kesi ya Ugaidi ya Mbowe.