Mwanamke aliyejioa nchini Uganda, Lulu Jemimmah hatimaye amepata ada ya kusoma chuo maarufu cha Oxford kilichopo nchini Uingereza.

Jemimmah, mwenye umri wa miaka 32, alikuwa anahitaji kiasi cha pauni 10,194 ili kumalizia mwaka wa pili na wa mwisho wa masomo yake ya uzamili.

Baada ya kuchangiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, amefanikiwa kupata pauni 11,160 ambayo ni pauni 966 zaidi ya lengo.

“Siyo tu nimepata pesa ya ada, kwa sasa sina haja ya kuwa na hofu yeyote ya kuhamisha fedha katika benki, usafiri wa ndege na pesa ya kuombea viza,” ameandika katika mtandao wake wa Go Fund Me Page

Aidha, ameongeza kuwa ukiacha mchango wa fedha, pia amepokea ufadhili wa tiketi za ndege kwa kipindi kilichobaki cha masomo yake kati ya Uingereza na Uganda

Hata hivyo, harusi ya mwanadada huyo ilimgharimu kiasi cha dola 2 tu ambazo ni gharama yake ya usafiri na aliazima gauni la harusi kwa rafiki, vito kutoka kwa dada yake na keki ya harusi iliokwa na kaka yake.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 14, 2018
Muungano wa vyama vya upinzani Congo DR wasambaratika