Mwanamke aliyewahi kuwa meneja wa Mariah Carey ameibua tuhuma dhidi ya mwanamuziki huyo kuwa alikuwa akimnyanyasa kingono kila walipokutana wakiwa wawili chumbani.

Stella Stolper ameiambia TMZ kuwa Mariah Carey alikuwa mtupu mara kadhaa na kumfanyia mambo ambayo ni ya kingono bila idhini yake.

Stolper ameiambia TMZ kuwa anafungua mashtaka rasmi dhidi ya mwimbaji huyo ili apate haki yake.

Aidha, Stolper anadai kuwa mbali na kumnyanyasa kingono, Mariah Carey aliwahi kukatisha mkataba wake wa miaka mitatu bila kufuata utaratibu na bila kumlipa kwa mujibu wa sheria.

Timu ya Mariah Carey imekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa wanasubiri kuitwa mahakamani kwa ajili ya kujitetea.

“Kama hiyo kesi ya tuhuma hizo zisizo na msingi itawasilishwa mahakamani, tutajitetea na tutashinda kirahisi,” walisema wawakilishi wake.

Hivi karibuni, Mariah Carey aliweka wazi kuwa ana tatizo la kisaikolojia la ‘bipolar disorder’, ambalo husababisha msongo wa mawazo. Ripoti iliyotolewa baadaye inaonesha kuwa Mariah alianza kutibiwa ugonjwa huo tangu mwaka 2001.

John Cena abwagana na mchumba wake
Mchezo kati ya Simba na Lipuli wapigwa kalenda

Comments

comments