Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijatambulika, amekutwa akiwa ananing’inia nusu uchi kwenye nyaya za umeme katika mitaa ya China, akikimbia fumanizi.

Kwa mujibu wa Daily Maily, chanzo kimeeleza kuwa mwanamke huyo anadaiwa alikuwa ndani ya chumba kimoja ghorofani na mume wa mtu. Lakini mke wa mwanaume huyo alirejea mapema zaidi ya walivyotarajia, hivyo aliamua kupitia dirishani kuokoa maisha yake.

Katika kipande cha video kilichosambazwa kwenye mitandao, umati mkubwa wa watu ulikuwa chini ukimtazama, kabla ya baadhi ya wanaume kuweka ngazi ili kumuokoa mwanamke huyo aliyekuwa ananing’inia akivalia mavazi mekundu.

Hata hivyo, haikufahamika mara moja kiasi cha maumivu au majeraha ambayo mwanamke huyo aliyapata kutokana na tukio hilo la hatari.
Magazeti ya Tanzania leo Julai 5, 2017

Video iliyowekwa mtandaoni kuhusu tukio hilo ilikuwa maarufu ndani ya muda mchache ikipata maelefu ya watazamaji.

Hata hivyo, kulikuwa na taarifa nyingine kinzani kuwa huenda mwanamke huyo alikuwa akisafisha madirisha ya nyumba hiyo, taarifa ambazo zimechukuliwa kama tetesi.

Video: Madareva 24 waliotekwa DRC, Wizara ya Mambo ya Nje yatoa tamko
Mshindi tuzo ya Uingereza afika bungeni