Mchekeshaji mahiri mwenye asili ya nchini Ghana, Marekani na Liberia Michael Blackson ameweka wazi mtazamo wake kuhusu umuhimu wa uaminifu katika maisha ya mahusiano ya Kimapenzi huku akibainisha imani yake juu jambo linaloweza kumfanya mwanamke awe tayari kumsaliti mwanaume tajiri na kukimbilia penzi la mwanaume asiye na uwezo wa kifedha ila muaminifu.

Akizungumza katika mahojiano maalumu Blackson alisema, “maisha yangu yote sijawahi kuwa mwaminifu, kwa yeyote kati ya marafiki zangu wa zamani waliokuwa wakitazama, niliwadanganya wote.

“Usaliti ni kwa wanaume matajiri kwa sababu wanaume wasio na uwezo hawawezi kumudu suala hilo, Wanaume masikini hawawezi kusaliti, wanaume masikini hawana chaguo, hawawezi kumudu hata wigi la mwanamke, atamudu vipi kufanya usaliti, atadanganya vipi?”.

Katika mazungumzo yake Blackson aliendelea kufafanua namna anavyolitazama jambo hilo kwa kusisitiza kuwa wakati mwingine mambo huwa tofauti ambapo wanawake wanaweza kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume tajiri mlaghai na msaliti, na kumuacha mwanaume masikini mwaminifu.

Ni upi mtazamo wako kuhusu usaliti unaosababishwa na kipato?

Wanaosambaza taarifa za uongo Chanjo ya Polio kupambana na Usalama
Mkataba wa Songas kupitiwa upya