Kamati ya waamuzi nchini imemteua mwamuzi Jonesia Rukyaa kupuliza kipenga katika pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga siku ya Jumamosi.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Jonesia kukabidhiwa jukumu la kuwa mwamuzi wa kati katika pambano hilo. Jonesia aliweka rekodi ya kuwa mwamuzi wa kwanza mwanamke kuchezesha mechi ya watani wa jadi nchini alipochezesha pambano la Nani Mtani Jembe mwaka juzi.
Jonesia atasidiwa na Josephat Bulali kutoka Tanga, Samwel Mpenzu (Arusha). Wakati mwamuzi wa akiba ni Elly Sasii kutoka Dar huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo kutoka Mwanza.