Je nini kikwazo kikubwa zaidi kwa mwanamke mwenye familia kutimiza ndoto zake za kielimu?

Kezia Mashingia ni jina Mashuhuri katika Chuo kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MweCau) Mkoani Kilimanjaro kwa kufundisha hapo kwa miongo kadhaa huku akiweka rekodi ya mwanamama mwenye umri mkubwa zaidi kupata shahada ya uzamivu nchini Tanzania na akiipatia katika chuo hicho alchofanyia kazi hadi kustaafu.

Wakati serikali ikiwaruhusu rasmi watoto wa kike waliopata ujauzito kurudi shule mara baada ya kujifungua ili kuweza kuendelea na masomo, Bibi Kezia anaipokea hali hiyo kwa kuonesha mfano mzuri kwa wanawake wenye watoto kujiendeleza kielimu ikiwa katika umri wake wa miaka 75 anahitimu masomo yake ya shahada ya uzamivu(PhD)katika chuo kikuu Cha kikatoliki Mwenge(MweCau).

Bi Kezia Mashingia (75)

Kezia ambaye ni mama wa watoto 8 na wajukuu 15 amesema aliamua kujiendeleza kimasomo mara baada ya kustaafu kazi rasmi serikalini akiwa na miaka 60 na akaendelea kufundisha katika chuo hicho huku akiwa anajiendeleza kimasomo kwa ngazi tofauti tofauti.

“Wakati naanza kufanya kazi nilikiwa na elimu ya shahada ya kwanza lakini pia nilikuwa na ndoto za kujiendeleza kimasomo jambo ambalo naona limefanikiwa licha ya kuwa tayari nina umri mkubwa”alisema Bi Mashingia

Anasema alipomaliza elimu ya msingi 1966 alijiunga na shule ya sekondari ya wasichana Tabora kati ya mwaka 1967-1968 na hatimaye alihitimu na kujiunga na jeshi mwaka 1969.

Baada ya hapo alijiunga na chuo kikuu mwaka 1972 akasoma astashahada ya uzamili katika elimu na alipohitimu akafanikiwa kufanya kazi katika vyuo mbalimbali vya elimu ikiwemo Mpwapwa,Chang’ombe sekondari ya Makumira na Vunjo.

“Huko kote nilikuwa nazunguka kumfuata mume wangu ila nikahamia chuo hiki kikuu Cha Kikatoliki Mwenge hadi 2006 nilipostaafu mwaka 2006 nikiwa na miaka 60″ameongeza Bi Mashingia

Bi Mashingia (75) amesema mara baada ya kustaafu alijiunga na chuo kikuu huria kwa masomo ya astashahada  kwa kipindi cha miaka 2 na alipohitimu akajiunga na shahada ya uzamili katika chuo cha Kikatoliki cha Mwenge na akajiunga tena na  chuo hicho kwa ngazi ya shahada ya uzamivu akiwa na umri wa miaka 70

Hivi kesho tarehe 27 Novemba anaenda kuhitimu huku kiu yake ikiwa ni kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na wanawake kupata elimu.

Afisa uhusiano wa chuo kikuu Kikatoliki cha Mwenge(MweCau)Atanas Sing’ambi amesema Kezia ni mmoja Kati ya wanafunzi 5 wanaoenda kuhitimu ngazi ya shahada ya uzamivu katika mahafali hayo ya 14 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Katika mahafali hayo yenye jumla ya wahitimu 851 Bibi Kezia Mashangai anapenyeza jina lake akiwa ni mwenye umri mkubwa zaidi kuzidi wahitimu wote lakini zaidi ni mwanamke alionesha mfano kuwa popote bila kuzingatia umri lengo la kielimu linaweza kutimia kwa mwanamke

B.1.1.529: Aina mpya ya Kirusi cha Corona inayoathiri vijana zaidi
Ulega asisitiza uzalishaji bora wa nyavu