Mpiga gitaa maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, Lokassa Kasia Denis (Lokassa ya Mbongo), amefariki dunia nchini Marekani alikokuwa akiishi baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kisukari.

Lokassa, ambaye hivi majuzi alifikisha umri wa miaka 80, alikuwa kiongozi wa bendi maarufu ya zamani ya Soukous Stars yenye makao yake makuu jijini Paris nchini Ufaransa na awali aliwahi kutamba na bendi ya Mwanamuziki Mkongwe Tabu Ley Rochereau, Afrisa International.

Mpiga gitaa maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, Lokassa Kasia Denis, ‘Lokassa ya Mbongo’.

Mwanamuziki mwenzake wa Kongo anayeishi Marekani, Mekanisi Modero alisema alikuwa amefahamishwa kuhusu kifo cha Lokassa na muuguzi ambaye amekuwa akimhudumia na kwamba alipatwa na matatizo ya kupumua kabla ya kuzimia na kufariki huko Nashua, New Hamsphire.

Mwimbaji Wawali Bonane amesema alimtembelea Lokassa na kusema amehuzunishwa na habari za kifo chake huku Mwanamuziki mwingine mkongwe wa DRC, Ngouma Lokito anayeishi New York, akitoa habari hiyo ya kusikitisha kwa mashabiki wake kupitia chapisho la mtandao wake wa jamii.

Lokassa ya Mbongo, (kulia), akiwa ameshikilia zawadi ya picha yake iliyochorwa na msanii wa DRC.

Hata hivyo, wengi wa Wanamuziki wa DRC akiwemo Lucien Bokilo, Swahiba wake na Marehemu Lokassa, Shimita El Diego, Ngouma Lokito na mume wa marehemu Tshala Muana, Claude Mashala wameoneshwa kusikitishwa na msiba huo mzito kwa Taifa la DRC.

RC Senyamule awavuta Mabalozi Dodoma
Simba SC, Azam FC, Young Africa zakwepana ASFC