Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Kasongo ‘Clayton’ Mpinda amefariki dunia.
Mpinda alikuwa akiimba kwenye bendi ya Wazee Sugu ‘La Capital’ inayomilikiwa na King Kiki.
Mpinda alikuwa akisumbuliwa na Kisukari na ganzi ya miguu. Mwanamuziki huyo ana asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mipango ya mazishi inafanywa.
Enzi za uhai wake amewahi kutamba na nyimbo kama Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine.