Taarifa za vyombo vya Habari nchini Jamhuru ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, zinasema Gwiji wa Muziki na mwimbaji mashuhuri, Elizabeth Amedeus Muidikay maarufu kama Tshala Muana amefariki Dunia.

Vyanzo vya habari vya Congo vinasema Tshala Muana amekumbwa na umauti asubuhi ya leo Jumamosi Desemba 10, 2022 jijini Kinshasa akiwa na umri wa miaka 64.

Aidha, Mume wa marehemu Tshala Muana, Claude Mashala pia amethibitisha kifo cha mwanamuziki huyo kupitia chapisho lake la mtandao wa Facebook bila kutoa sababu za kifo chake, ambapo Juni, 2020 kulitokea uvumi kuwa amefariki baada ya kulazwa Hospitalini kufuatia kuugua ugonjwa wa kiharusi.

Elizabeth Amedeus Muidikay, “Tshala Muana” May 13, 1958 – Desemba 10, 2022. Picha ya Spotfy.

Claude ameandika kuwa, “Asubuhi na mapema Mola mwema alichukua uamuzi wa kumchukua Mamu Tshala Muana wa kitaifa. Mungu mwema atukuzwe kwa nyakati zote njema alizotujalia hapa duniani. Kwaheri Mamu kutoka.”

Marehemu Muana alizaliwa May 13, 1958 huko Lubumbashi, DRC na anajulikana kwa mtindo wake wa Mutuashi na utunzi wa nyimbo kadhaa zilizovuma katika bara zima la Afrika na ulimwengu kiujumla, ukiwemo wa Tshibola, Karibu Yangu, Kakola, Dezodezo na nyinginezo.

Waliofutiwa matokeo kurudia mtihani
Watoto 80 waachiliwa, kesi bado inaendelea