Msanii wa muziki nchini Uingereza Marcus Birks(40) amefariki dunia akiwa hospitali anatibiwa Corona.

Birks alikua ni katika watu waliokataa kupata chanjo ya Corona kwa kusema hawezi kuupata ugonjwa huo kwa kuwa anafanya mazoezi mara tano kwa wiki na alikua anakula vizuri kwa kuzingatia lishe bora.

Baada ya kupata Corona mapema mwezi agosti Birks wakati akiongea kwenye mahojiano aliyoyafanya, alionyesha kujutia maneno yake na kuwashauri watu wote ambao hawajachanjwa kutopuuzia chanjo hiyo na kutosikiliza maneno ya watu bali kujali afya zao.

Birks amefariki na kuacha mke akiwa mjamzito.

STAMICO yapata dili la Bilioni 4
Mtambo wa kukausha mbao wazinduliwa