Siku Chache zilizopita Polisi kaskazini mashariki mwa Nigeria walikuwa wakimtafuta mwanamuziki mmoja maarufu Ado Daukaka ambaye alitoweka siku ya Ijumaa.

Mwanamuziki huyo aliripotiwa kutoweka baada ya kutoa wimbo unaozungumzia kushindwa kwa majukumu na ufisadi miongoni mwa wabunge.

Mmoja wa wake zake aliiambia BBC kuwa Daukaka alitembelewa na watu wasiojulikana saa za asubuhi, siku ya Ijumaa na huo ndio wakati wa mwisho familia yake

Hata hivyo Polisi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wamempata msanii huyo aliyepotea siku ya ijumaa na kusema wamemkuta akiwa katika hali ya kutokuwa na fahamu huku akiwa amedhoofu  sana.

Daukaka ameiambia BBC kuwa alitekwa nyara na kundi la watu waliokuwa na hasira kutokana na wimbo aliouandika uliokuwa unawazungumzia viongozi wa siasa wanaojihusisha na rushwa.

Amesema walimuweka ndani kwa siku mbili bila ya kumpatia chakula na kisha kumtelekeza msituni.

Kwa sasa anaendelea na matibabu katika hospitali moja iliyopo kilomita 120 kutoka eneo alilotekwa.

Mojawapo ya nyimbo zake ni unaoitwa kwa lugha ya Kihausa Gyara kayanka, ukimaanisha ”tunapaswa kufanya matendo mema” unaowazungumzia wanasiasa wanaotoa ahadi nzuri bila kuzitimiza.

Kokosi Cha Twiga Stars Chaanikwa Hadharani
Video: Tundu Lissu Mbaroni. JPM ammwaga DC Ikulu. Lamwai aibuka na 'Askari' wa Lowassa - Magazeti