Mwanariadha wa mbio za marathoni wa Ethiopia, Feyisa Lelisa, aliyeshinda medali ya fedha katika michuano ya Olimpiki ya Rio 2016 iliyomalizika mwishoni mwa juma lililopita, amezusha habari duniani kwa kuonyesha ishara ya kugomea yanayofanyika katika eneo la Oromia nchini Ethiopia.

Ishara hiyo ya kisiasa inamuweka mwanariadha huyu mashakani na sasa baadhi ya Wa-Ethiopia wanaoishi nje wanataka kumsaidia.

Solomon Ungashe anayeishi jimboni California ni mmoja wa watu watatu waliofungua akaunti ya mtandaoni ya kumsaidia mkimbiaji huyo.

Ungashe ameiambia VOA kwamba mwanariadha huyo hakuomba kufanyiwa hilo lakini washabiki wake ndio walioamua baada ya kuona haja ya kufanya hivyo, na wamefanikiwa kukusanya dola za kimarekani 100,000 mpaka sasa.

Wameshatuma watu watatu kwenda jijini Rio de Jeneiro, Brazil, kumpatia msaada.

Mkwasa Atangaza Kikosi Cha Taifa Stars, Awatema Ulimwengu, Juma Abdul
Yanga Yaushtukia Uwanja Wa Uhuru, Viongozi Washauriwa Kitaalam