Jeshi la Polisi jijini Nairobi linamshikilia mwanasheria mwandamizi, Issa Nyakundi aliyempiga risasi kifuani mwanaye wa kiume mwenye umri wa miaka  29.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mwanasheria huyo alimpiga risasi mwanaye huyo wa kumzaa alityetajwa kwa jina la Joseph, kwa bahati mbaya alipokuwa akijaribu kuitunza bastola yake wakiwa ndani ya gari.

Imeripotiwa kuwa Nyakundi alikuwa na mwanaye kwenye gari wakirejea nyumbani majira ya saa saba usiku, walipokuwa wakitoka kwenye ibada katika kanisa la ICC, walipokaribia nyumbani wakiwa kwenye barabara ya Mombasa, mwanasheria huyo aliitoa bastola yake na kujaribu kuiweka kwenye mfuko wake maalum lakini risasi ilifyatuka bahati mbaya.

Alimkimbiza mwanaye kwenye hospitali ya Agha Kahan iliyokuwa karibu, lakini alipofika madaktari walimueleza kuwa tayari Joseph alikuwa ameshapoteza maisha.

Polisi wameeleza kuwa Nyakundi alikuwa raia anayemiliki bastola hiyo kihalali na kwamba wanamshikilia yeye na bastola yake kwa ajili ya kusaidia upelelezi.

Mo Dewji ateta na kocha wa Simba, afunguka
Nassari amlilia Ndugai, 'Alihudhuria harusi yangu, bado ana nafasi ya kurejea uamuzi wake'

Comments

comments