Mwanasheria wa Chris Brown, Mark Geragos amepinga vikali tuhuma za ubakaji zilizotolewa na mwanamke mmoja hivi karibuni dhidi ya mwimbaji huyo, akidai kuwa ni uzushi wa njaa ya fedha.

Hivi karibuni, mwanamke mmoja alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kuwa Chris alinyanyasa kingono alipokuwa nyumbani kwake.

Hata hivyo, mwanasheria wa Chris amesisitiza kuwa kama madai haya yote yangekuwa kweli, basi  ni lazima uchunguzi wa kosa la jinai ungeanza kufanywa na jeshi la polisi.

Alisema kuwa anashangazwa na kitendo cha mwanamke huyo kudai kuwa anataka alipwe fidia ya  $17 milioni, kwani hizo ni kama kuanzisha tuhuma za njaa ya fedha.

“Ukweli ni kwamba aliniambia anataka alipwe  $17 milioni, na mimi nikawaambia waende zao wakaeleze kwanza ni kwanini waliamua kuita vyombo vya habari,” alisema Geragos. “Chris hajafanya kosa lolote, na wanajua dhahiri kuwa hajafanya kosa lolote,” alisisitiza.

Alisema kuwa mteja wake huyo amekuwa akiandamwa na kesi za aina hiyo kutoka kwa watu ambao wanataka kulitumia jina lake kufanya mambo yao.

Mei 4, mwanamke mmoja alijitokeza mbele ya vyombo vya habari akieleza kuwa alibakwa na mwanaume alipokuwa nyumbani kwa Chris Brown. Aliongeza kuwa alilazimishwa kufanya ngono ya mdomo na mwanamke mmoja aliyemkuta kwenye nyumba hiyo ambaye alikuwa ‘kwenye siku zake’.

 

Usifanyie hiki mshahara wako
Makomando wa Marekani wawakamata Al-Shabaab