aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Bitaho (54) amehukumiwa kulipa faini ya Shilingi milioni 13.9 au kifungo cha jela miaka mitano baada ya kusomewa upya mashtaka na kukiri kosa.
Bitaho ambaye ni Raia wa Burundi alifutiwa mashtaka yake na baadae kukamatwa teana na kusomewa hukumu hiyo na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.
Akisoma hukumu hiyo Nongwa amesema kuwa mahakama imesikiliza maombi ya pande zote mbili na kwamba katika kosa la kwanza hadi la saba mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Shilingi laki tano au kifungo jela kuanzia miaka miwili hadi mitatu na kwamba kosa la nane mshitakiwa atatakiwa kulipa  faini ya Shilingi milioni 10 au kifungo jela miaka mitano.
Amesema kuwa kwa taratibu zilizopo, baada ya mshitakiwa kukutwa na hatia anatakiwa kupelekwa Uhamiaji na kurudishwa nchini kwao ili aombe uraia wa Tanzania upya.
Aidha, akimsomea maelezo ya awali (PH), baada ya kukiri mashtaka yake, Mwendesha Mashitaka wa Uhamiaji, Method Kagoma amedai kuwa wazazi wa Bitaho waliingia nchini mwaka 1958 na kisha kurudi tena mwaka 1972 huku yeye Bitaho akiwa mtoto mdogo.
Hata hivyo, Kagoma amedai kuwa, Oktoba 19, 2013 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wilayani Ilala Dar es Salaam, akiwa mkimbizi na Raia wa Burundi, alishindwa kutimiza masharti yaliyotolewa Septemba 11, 2013 na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji ambapo alishindwa kurejesha hati ya kusafiria aliyoipata isivyohalali.

Makamba atoa agizo kwa wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi nchini
Video: JPM ashtusha, Kiama viwanda 179